WAZEE WA WILAYA YA RORYA WALIA NA VIJANA WANAOKOSA ELIMU YA FEDHA

Baadhi ya Wazee wa Kijiji cha Nyasoko na Nyanduga Kata ya Koryo, Wilayani Rorya Mkoani Mara m, wameeleza shauku yao ya kuona elimu ya fedha inawafikia zaidi vijana ambao wanatafuta fedha kwa bidii lakini hawaendelei kiuchumi kutokana na kukosa elimu ya fedha. Hayo yameelezwa na Wazee wa Vijiji hivyo akiwemo Mzee Cleophas Otieno Obelo, Ray Abich na Mchungaji Thomas Msoke, wakati Timu ya Wataalamu wa elimu ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, ikiongozwa na Bw. Salim Khalfan Kimaro ilipofika katika kata hiyo, kutoa elimu ya fedha.