WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO

Watumishi wa Wizara ya Fedha wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia sheria, kanuni, taratibu pamoja na miongozo katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya wizara ili kuleta tija katika Taasisi na Taifa kwa ujumla. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, wakati akifungua kikao kazi cha Watumishi wa Wizara hiyo kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini - IRDP, jijini Dodoma.