WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WAJIVUNIA UTALII WA NDANI
Watumishi wa Wizara ya Fedha wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Bw. Lusius Mwenda, wametembelea Kituo cha Kihistoria cha Magofu ya Kaole, Bagamoyo mkoani Pwani kujionea vivutio vya utalii vilivyoko eneo hilo.
Watumishi hao wamefanya utalii wa ndani ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa 38 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha, ambao umekutanisha Wajumbe kutoka Makao Makuu ya Wizara, Wakuu wa Hazina Ndogo na Wahakikimali kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara.