WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WAHIMIZWA MICHEZO KWA AFYA, KUONGEZA UFANISI
Watumishi wa Wizara ya Fedha na Taasisi zilizo chini yake wamehamasishwa kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya zao na kuongeza ufanisi katika majukumu yao.
Rai hiyo imetolewa katika viwanja vya Mlimani jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Dkt. Vedastus Timothy alipozindua Bonanza la michezo lililoandaliwa na Wizara ya Fedha na taasisi zilizo chini yake kwa kushirikiana na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).