WATUMISHI WAASWA MAADILI NA WELEDI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi, Jenifa Omolo, ameshiriki hafla fupi ya kuwaaga Maafisa Usafirishaji wa Wizara hiyo waliostaafu kazi hivi karibuni, ambapo aliwashukuru watumishi hao kwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili muda wote walipokuwa kazini. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Royal Village, jijini Dodoma.