WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA WASHIRIKI MEIMOSI DODOMA.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha, wameshiriki sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), ambapo kwa ngazi ya Mkoa wa Dodoma yamefanyika katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Maadhimisho ya Siku hii ya Wafanyakazi Duniani kitaifa, yamefanyika katika Mkoa wa Njombe ambapo pia baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha wameshiriki sherehe hizo.
