WATUMISHI WA UMMA WAASWA KUWEKEZA KABLA YA KUSTAAFU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Omolo amewataka watumishi wa Umma kutimiza majukumu yao kwa wakati na weledi na kuwekeza kwa ajili ya Maisha ya uzeeni ili kuepuka usumbufu katika kipindi cha kustaafu. Bi. Omolo ametoa wito huo wakati wa mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Fedha mwaka 2023/2024, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika ukumbi wa Kilimanjaro, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar Es Salaam.