WATOA HUDUMA ZA FEDHA WASHAURIWA KUWAELIMISHA WATEJA KABLA YA KUTOA HUDUMA
Watoa Huduma za Fedha wameshauriwa kuwapa elimu wateja wanaowahudumia ili wapate uelewa wa masharti ya mkopo ikiwemo muda wa mkopo, riba na kiwango cha kurejesha kabla ya kuchukua mkopo na kusaini mkataba ili kupunguza migogoro inayoweza kutokea baada ya huduma kutolewa.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Mikopo wa Taasisi ya Tofo Financial Services Bw. Dastan Sebastian, ambae ni mkazi katika Kata ya Mutukula wilayani Missenyi mkoani Kagera, baada ya kupata elimu ya masuala ya fedha inayoendelea kutolewa na Timu ya Wataalamu ya Wizara ya Fedha ambayo ipo mkoani Kagera kwa ajili ya kutoa elimu hiyo kwa wananchi wa makundi mbalimbali.