WATOA HUDUMA ZA FEDHA WAONYWA UVUNJAJI SHERIA

Watoa huduma za fedha mkoani Manyara wametakiwa kufuata sheria na taratibu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ikiwemo kujisajili, kutoza viwango sahihi vya riba na kuwapa nakala za mikataba wakopaji baada ya wao kuelewa mkataba wa makubaliano ya kukopa na kusaini ili kuepuka adhabu mbalimbali zitakazotolewa kwa wanaokiuka sheria za huduma za fedha. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bi. Queen Sendiga, ofisini kwake alipokutana na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha kabla hawajaingia kwenye kikao cha Baraza la Biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, kutoa elimu ya fedha kwa wajumbe wa kikao hicho.