WATOA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA TURIANI WATAKIWA KUFUATA SHERIA.

Watoa huduma ndogo za fedha katika tarafa ya Turiani Mkoani Morogoro wametakiwa kutoa huduma hizo kwa wananchi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa na serikali. Akizungumza katika mfufulizo wa program ya kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya fedha, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mtibwa kaika tarafa ya Turiani, Wilayani Mvomero, Bi. Rudhaa Antony alisema baadhi ya Taasisi zilizopo katika tarafa hiyo zimekuwa zikitoa huduma bila ya kuzingatia taratibu zilizowekwa kwa kutoa huduma hizo kwenye magari badala ya kuwa na ofisi rasmi ya kutolea huduma hizo.