WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA BENKI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewataka Watanzania kutumia benki kuhifadhi fedha zao ili kuhakikisha usalama wa fedha zao na usalama wao na kuacha tabia ya kuhifadhi fedha majumbani.
Dkt. Nchemba aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akizundua Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo na kushindwa kutokana na majukumu mengine ya Kitaifa.