WATAALAMU WA UBIA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAJADILI UBIA

Wataalamu kutoka Kitengo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), na Wataalam kutoka Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Zanzibar, kupitia Idara ya Mashirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPD), wamekutana na kujadili kuhusu maandalizi ya Kikao cha Kwanza cha Ushirikiano kati ya pande zote mbili kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar Es Salaam. Katika kikao hicho wataalamu hao walijadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitia na kuthibitisha ajenda zitakazojadiliwa katika Kikao cha Kwanza cha Ushirikiano huo.