WATAALAMU WA MASUALA YA FEDHA WATAKIWA KUWAONDOLEWA CHANGAMOTO WANANCHI
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Ruth John amewaomba watalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na sekta ya fedha nchini kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hasa watumishi wa umma zinazotokana na upatikanaji wa huduma za fedha zisizo rasmi.
Bi. Ruth aliyasema hayo wakati Timu ya program maalum ya elimu ya fedha kwa umma kutoka Wizara ya Fedha na washirika kutoka sekta ya fedha nchini walipofika ofisini kwake kabla ya elimu hiyo kutolewa kwa wakazi wa Morogoro mjini.