WASTAAFU WAONYWA KUHUSU MATAPELI

Wizara ya Fedha imeendelea kuwakumbusha wastaafu wanaolipwa mafao na Wizara ya Fedha kutojihusisha na utoaji wa fedha kwa mtu, kama kigezo cha kusaidiwa kupata mafao yao, Kwakuwa huduma hiyo hutolewa bure. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ambaye pia ni Msemaji wa Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja, wakati akifungua kongamano la Elimu kwa Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii nchini liliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa NaneNane mjini Morogoro.