WASHIRIKA WA MAENDELEO WAOMBWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI

Serikali imewahimiza washirika wa maendeleo kushiriki katika kuwezesha nchi kufufu fursa zote za kiuchumi zilizozuiwa na kuharibiwa na athari za Uviko- 19 pamoja na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraini. Wito huo umetolewa na Makamu wa kwanza wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika katika Hotel ya Seaclif, Zanzibar.