WANANCHI WATAKIWA KUFAHAMU MNYORORO WA UGAVI

Wananchi wametakiwa kufahamu mnyororo wa ugavi ambao ni sehemu muhimu yenye mchango mkubwa katika kufanikisha malengo ya Serikali hasa katika nyanja za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hayo yamesemwa na Afisa Ugavi Mwandamizi kutoka Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Bi. Vaileth Mwakajisi (wa pili kulia) alipokuwa akitoa elimu kuhusu mnyororo wa ugavi kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.