WANANCHI WAMIMINIKA KUPATA ELIMU BANDA LA WIZARA YA FEDHA- SABASABA
Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanakopa katika maeneo rasmi ili kuondoa changamoto ya mikopo umiza ambayo imekuwa ikileta adha kwa wananchi kwa kufilisiwa mali zao.
Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) Afisa Mwandamizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo amesema Serikali imeweka utaratibu wa kujisajili kwa watoa huduma za fedha ili kukomesha tatizo hilo.