WANANCHI WA WILAYA YA BUSEGA WAPEWA ELIMU YA HUDUMA YA FEDHA
Picha za matukio mbali mbali ya mafunzo ya elimu ya fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, elimu hiyo ya fedha ilianza kutolewa maeneo ya mijini kupitia maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kwa Mikoa ya Dar Es Salaam, Mwanza na Arusha, ambapo kwa sasa programu hiyo imejikita kuwafikia wananchi wote kwa lengo la kuwaongezea uelewa wa masuala ya fedha ili waweze kufanya maamuzi sahihi katika mahitaji na matumizi ya huduma za fedha maeneo mengine yaliyofikiwa ni pamoja na Mkoa wa Manyara, Singida, Kagera, Rukwa, Kigoma, Tabora na Simiyu.