WANANCHI WA TARAFA YA MIKESE WAISHUKURU SERIKALI KUWAFIKISHIA ELIMU YA FEDHA

Wananchi wa Tarafa ya Mikese Mkoani Morogoro wameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa kuwapitia elimu ya fedha ambayo inatolewa kupitia Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 – 2029/30. Wananchi hao walisema kuwa elimu inayotolewa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya fedha nchini imekuwa na msaada mkubwa katika Tarafa ya Mikese baada ya wananchi wa Kata hiyo kusumbuka kwa muda mrefu kutokana na baadhi ya watu wasio waaminifu kutoroka na fedha zao walizokuwa wanawekeza kupitia vikoba visivyo rasmi.