WANANCHI WA MLIMBA WAMSHUKURU MHE. SAMIA KUWAFIKISHIA ELIMU YA FEDHA

Wananchi wa Halmashauri ya Mlimba Mkoani Morogoro wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka na kuwafikishia elimu ya fedha ambayo itawasaidia wananchi waishio vijijini kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali ya fedha yakiwemo ya uwekezaji na mikopo. Akizungumza katika mfufulizo wa program ya elimu ya fedha kwa umma inayoendeshwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikia na washirika wa sekta ya fedha nchini, Diwani wa kata ya Ching’anda katika Halmashauri ya Mlimba Mhe. Hassan Kidapa amesema kupitia elimu iliyotolewa wananchi watakwenda kunufaika hasa katika kupanga mipango na kuitumia vizuri.