WANANCHI WA KAGERA WAISHUKURU SERIKALI KUWAFIKIA

Wananchi wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Fedha kwa kuwafikishia huduma ya elimu ya fedha itakayowakomboa kiuchumi na kuwaepusha na upotevu wa fedha. Shukrani hizo zimetolewa na wananchi hao baada ya kumalizika kwa semina ya elimu ya fedha iliyotolewa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha iliyofanyika katika Ukumbi wa Kashura “Women Centre” uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.