WANANCHI WA BIHARAMULO WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA ELIMU YA FEDHA
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Advera Bulimba, amewataka Wananchi wilayani Biharamulo kujitokeza kwa wingi ili wapate elimu ya fedha itakayowakomboa kiuchumi kwa ustawi wa jamii na nchi kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa na SACP Bulimba, alipokutana na Timu ya wataalamu ya Wizara ya Fedha ambao wanaendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali katika Wilaya nne za Bukoba, Missenyi, Muleba na Biharamulo mkoani Kagera.