WANANCHI NGORONGORO WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WATAALAMU WA TATHMINI YA KITUO CHA FORODHA.

Wananchi wa Ngorongoro mkoa wa Arusha wametakiwa kutoa ushirikiano kwa wataalamu wanaofanya tathmini ya uhitaji wa kuanzishwa kwa Kituo cha Huduma za Forodha katika eneo hilo, ili kubaini iwapo eneo hilo linakidhi vigezo vya kisheria na kiutendaji vya kuwa na kituo hicho. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Njoroi, Kata ya Ololosokwan, Tarafa ya Loliondo katika mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo linalopendekezwa kuwa na Kituo cha Forodha.