WANANCHI EPUKENI MADENI YASIYO YA LAZIMA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza, Bw. Mohammed Kiande, amewataka wananchi kupanga matumizi yao vizuri, kuepuka madeni yasiyokuwa ya lazima, kujenga utajiri na kuongeza Uelewa wa Masuala ya kiuchumi. Bw. Kiande alitoa rai hiyo wakati alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, Taasisi za Serikali na Binafsi ambayo ipo mkoani Mwanza kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali.