WALIPAKODI NA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA KUSULUHISHWA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameiagiza Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za kodi (TOST) kuhakikisha inatatua migogoro mbalimbali ya kodi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kukusanya mapato pamoja na kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara nchini. Dkt. Nchemba alitoa agizo hilo Jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Ofisi hiyo mpya ambayo iko chini ya Wizara ya Fedha.