WALIOCHUKUA KADI ZA BENKI ZA WATUMISHI KINYUME NA SHERIA KUBANWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, Bw. Abdul Mtaka, ametoa agizo kwa taasisi zenye tabia ya kushikilia kadi za benki za watumishi wa Umma kama dhamana wanapokopa kuacha mara moja vitendo hivyo kwa kuwa ni kinyume cha Sheria. Agizo hilo amelitoa Wilayani Rorya alipotembelewa na Timu ya Wataalamu wa Elimu ya Fedha ikiongozwa na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, iliyofika kwa ajili ya kutoa elimu katika Wilaya hiyo. Bw. Mtaka alisema kuwa ameandaa Timu inayo kusanya taarifa ya vitendo hivyo na baada ya kukamilika hatua mbalimbali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria zilizopo.