WAKUU WA VITENGO VYA MAWASILIANO WAASWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI

Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano vya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, wameaswa kuendelea kutangaza majukumu yanayofanywa na taasisi zao kikamilifu ili kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu miradi ama kazi zinazotekelezwa na Taasisi hizo na kuchangia kukuza uchumi na maendeleo ya nchi. Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati akifungua Kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano na Masoko vya Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari lililofanyika katika Ukumbi wa Nanenane, Mkoani Morogoro.