WAKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO WAFANYA MAPITIO YA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA
Serikali kupitia Wizara ya Fedha, imefanya kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta, ikiwa ni sehemu ya mchakato endelevu wa kuboresha utekelezaji wa bajeti na kuhakikisha uwazi, tija na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma.
Akifungua kikao kazi hicho, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha Bw. Moses Tesha, alisema kuwa Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review- PER) ni takwa la kisheria chini ya Sheria ya Bajeti Sura ya 439 na Kanuni zake, na hufanyika kila mwaka wa fedha.
