WAKULIMA WA KASKAZINI KUNUFAIKA NA MIKOPO YA BENKI YA TADB

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameiagiza Menejimenti ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) iweke masharti nafuu ya mikopo ili kuwezesha wakulima, wavuvi na wafugaji kupata mikopo hiyo kwa wakati na kwa gharama nafuu. Dkt. Nchemba alitoa rai hiyo jijini Arusha wakati akizinduzi Ofisi ya Kanda ya Kaskazini ya Benki ya hiyo itakayohudumia mikoa ya ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga.