WAKAZI WA MLIMBA WASHAURIWA KUTUMIA TAASISI ZILIZO RASMI KUPATA HUDUMA ZA FEDHA.

Wakazi wa Halmashauri ya Mlimba, Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro wametakiwa kuhakikisha wanatumia Taasisi za huduma ndogo za fedha ambazo zimeidhinishwa kisheria kufanya shughuli hizo nchini kwa mujibu wa Sheria. Akizungumza katika program ya elimu ya fedha inayoendeshwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Fedha nchini, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlimba Neuster Ngelela, alisema kuwa ili kupunguza migogoro kati ya wananchi na watoa huduma ndogo za fedha ni vyema wananchi wakajielekeza kupata huduma hizo katika Taasisi za fedha zilizo rasmi na zilizosajiliwa na kupewa leseni ya kuendesha shughuli hizo.