WAKAZI WA KASELYA WILAYANI IRAMBA WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI

WAKAZI wa Kata ya Kaselya Wilayani Iramba mkoani Singida wameondoka na na adha ya maji baada ya kukamilika kwa mradi wa Maji wa Kaselya uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 770. Wakazi hao wameishukuru Serikali kwa kufanikisha na kukamilisha ujenzi wa mradi huo, wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alipotembelea na kukagua mradi huo ambao fedha zake zinatokana na mradi wa kukabiliana na athari za UVIKO 19.