WAKAZI WA KAGERA KUONDOKANA NA ADHA YA NISHATI YA UMEME BAADA YA AFDB NA AFD KUTOA FEDHA
WAKAZI wa Mkoa wa Kagera wanatarajia kuondokana na changamoto ya kukosa umeme wa uhakika baada ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB na Shirika la Maendeleo la Ufaransa kusaini mikataba ya mkopo yenye masharti nafuu ya dola za Marekani milioni 161.47 na euro milioni 110, mtawalia, sawa na shilingi bilioni 647.5 za Tanzania.
Mikataba imesainiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwa upande wa Tanzania, Meneja wa Benki ya Maendeleo ya Afrika nchini Tanzania Dkt. Patricia Laverley na Bi. Celine Robert, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa-AFD.