WAKAGUZI WA NDANI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUBORESHA TAARIFA ZA FEDHA

Jumla ya wakaguzi 120 wa ndani wa taarifa za fedha wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukagua taarifa za fedha ili kuhakikisha taarifa za fedha zinaandaliwa kwa viwango vya kimataifa. Akizungumza wakati wa Kufunga mafunzo hayo, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Benjamin Magai, alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuboresha utendaji wa wakaguzi wa ndani ili kuzishauri menejimenti za taasisi husika kuhusu usahihi wa taarifa hizo kabla hazijawasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).