WAHITIMU CHUO CHA MIPANGO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII

Serikali imewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kutumia ujuzi na mafunzo waliyoyapata kujiajiri badala ya kutegemea ajira rasmi pekee ili kujikwamua kimaisha. Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo ambaye alimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika mahafali ya 36 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.