WAHITIMU CHUO CHA MIPANGO WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA ZABUNI ZA UMMA
Serikali imewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kuchangamkia fursa ya upendeleo inayotolewa na sheria ya manunuzi inayozitaka taasisi zote za Serikali kutenga asilimia 30 ya bajeti zao za manunuzi ya mwaka kwa ajili ya makundi maalum katika jamii wakiwemo vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.