WAFICHUENI KAUSHA DAMU ILI KUIONDOA JAMII KWENYE MATATIZO

Kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa Elimu ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro amewataka wakazi wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, kutoa taarifa kwa Mamlaka husika inapobainika uwepo wa mtoa huduma ndogo za fedha asiyesajiliwa na anayetoa huduma kinyume cha Sheria. Rai hiyo imetolewa wakati wa zoezi la kutoa elimu ya fedha katika maeneo ya Manga, Sirari, Matombo, Nyamwaga, Ganyange na Gorong’a, yaliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.