WADAU WA UKUSANYAJI MAPATO YASIYO YA KODI WAPIGWA MSASA

Serikali imezitaka wizara, idara zinazojitegemea na taasisi za Serikali zinazokusanya Mapato yasiyo ya kodi, kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia malengo ambayo Serikali imejiwekea kwaa mwaka wa fedha 2022/2023. Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma na Kamishna wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Elijah Mwandumbya, wakati wa Semina ya taratibu za ukusanyaji wa Mapato yasiyo ya kodi iliyowakutanisha maafisa mipango, TEHAMA, wahasibu na wakaguzi wa ndani.