WADAU WA MITANDAO YA KIJAMII WAPEWA ELIMU YA KODI

Wadau wa Mitandao ya Kijamii wameaswa kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti halali zinazolingana na kiasi cha fedha walichotoa kila wanapofanya manunuzi na kutoa risiti wanapo uza bidhaa na huduma. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, wakati akifungua Kongamano la wadau wa mitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 hadi 24 Oktoba, 2023.