VIKUNDI VYATAKIWA KUJISAJILI VIWEZE KUTAMBULIKA
Vikundi mbalimbali vinavyotoa huduma za fedha zimetakiwa kusajili vikundi vyao ili viweze kutambulika rasmi na Serikali ili kupata uhalali wa kisheria na sifa ya kupata mikopo na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali.
Wito huo umetolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Nachingwea, Bi. Amina Ally Said, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, iliyopo mkoani Lindi kutoa elimu ya masuala ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali.