VIKUNDI VYA KIJAMII VYASHAURIWA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA WEZESHA PORTAL.
Vikundi vya Kijamii na huduma ndogo za fedha nchini vimetakiwa kujisajili katika mfumo wa wezesha portal ambao umeanza kutumika tangu mwezi Oktoba, 2023, ili kuweza kungiza taarifa za vikundi hivyo ikiwemo taarifa za biashara zao, namna wanavyokopa na kufanya marejesho ya mikopo yao.
Akizungumza katika mwendelezo wa program ya elimu ya fedha kwa umma iliyotolewa kwa wananchi wa Halashauri ya Manispaa ya Morogoro, Kamishina Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta Ndogo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, alisema ni muhimu watoa huduma ndogo za fedha wakajisajili na kupata leseni ya kutoa huduma hizo kwa wananchi kwa mujibu wa sheria za Benki Kuu ya Tanzania.