UNICEF YAAHIDI KUWEKEZA TANZANIA KATIKA LISHE KWA WATOTO
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), limeahidi kuisaidia Tanzania kwenye masuala ya Lishe ili kukabiliana na Udumavu wa watoto ambao unaathari katika ukuaji wa ubongo na uchumi.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Bi. Elke Wisch, jijini Dodoma.