UMOJA WA ULAYA WAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 380

Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia Tanzania msaada wa euro milioni 166 sawa na takribani shilingi za Tanzania bilioni 380 ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ikiwemo kuibua fursa zitokanazo na bahari (uchumi wa buluu), sekta Jumuishi ya fedha na kuimarisha ushirikiano. Msaada huo umetangazwa leo tarehe 26 Oktoba, 2022 Jijini Dar es Salaam mbele ya wanahabari na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Kamisheni ya Ulaya Mhe. Jutta Urpilainen na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.