UJUMBE KUTOKA ZANZIBAR WAPATA MAFUNZO KUHUSU PPP

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, amekutana na ujumbe wa Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Rashid Ally Salim, katika kikao kazi kilichojadili kuhusu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) majukumu ya Kitengo cha PPP, masuala mbalimbali kuhusu Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.