UJERUMANI YAAHIDI KUSAIDIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

Tanzania na Ujerumani zimesaini Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria. Makubaliano hayo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen.