UJENZI WA DARAJA LA JUU JANGWANI KUANZA HIVI KARIBUNI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewataka Wakala wa Barabara nchini -TANROADS kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa Mkandarasi atakayejenga Daraja la Mto Msimbazi ili kuwaondolea wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, changamoto ya mafuriko. Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo baada ya kuongoza Ujumbe wa Serikali na Benki ya Dunia kutembelea eneo la Jangwani ambapo mradi wa uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi, unatarajiwa kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa daraja kubwa la juu la Jangwani, kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mapema mwakani, kwa gharama ya zaidi ya dola za marekani milioni 350.