UINGEREZA KUSAIDIA TANZANIA SEKTA YA AFYA
Tanzania na Uingereza zimesaini hati za Makubaliano ya nyongeza ya kuchangia Mfuko wa Kusaidia Sekta ya Afya (Health Basket Fund (HBF)) kati ya Serikali na wadau wa maendeleo (Development Partners) ya pauni milioni 10 (sawa na Tsh bilioni 34), itakaowezesha utoaji wa huduma bora za afya nchini kuanzia mwaka 2024 hadi 2029.
Hati hizo zimesainiwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John A. Jingu, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Grace E. Magembe na Mkurugenzi wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini, Bi. Olukemi Williams, hafla iliofanyika katika ukumbi wa ofisi za Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).