TIA YATAKIWA KUONGEZA WIGO WA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZAKE NCHINI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), ameitaka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha miundombinu iliyopo inatumika kuhakikisha kampasi zote saba zinapata wanafunzi.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, katika Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw Elijah Mwandumbya, ameitaka Taasisi ya TIA kuweka mikakati ya kuhakikisha taarifa zinawafikia watanzania wote popote walipo ndani na nje ya nchi ili watumie fursa za kujiendeleza kielimu kupitia kozi mbalimbali, zinazotolewa kwenye Chuo.