TASAF KUNUFAIKA NA MSAADA WA SH. BIL 15 KUTOKA UINGEREZA

Tanzania imepokea msaada wa paundi milioni tano sawa na takribani shilingi bilioni 15 kutoka Serikali ya Ungereza kwa ajili ya awamu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF). Makabidhiano ya Hati za makubaliano ya msaada huo yamefanyika jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar.