TANZANIA YAUNGA MKONO TAMKO LA CHINA KUHUSU UJENZI WA MIUNDOMBINU WEZESHI YA BIASHARA KWA NJIA MBADALA

Tanzania imeunga mkono hatua ya China ya kusisitiza umuhimu wa kutumia njia mbadala ya kutoa mikopo na misaada kwa nchi zinazoendelea zikiwemo za Afrika kwa kuishirikisha sekta binafsi ili kuchochea kasi ya ujenzi wa miundombinu kupitia mpango wake wa Belt and Road Initiative (BRI). Kauli hiyo imetolewa Jijini Beijing, nchini China na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maanry Mwamba, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Tatu la Kimataifa la Belt and Road Initiative, ulioyakutanisha mataifa kadhaa duniani, ukibeba kaulimbiu ya kuimarisha uchukuzi ili kukuza Biashara (Trade & Connectivity')