TANZANIA YATETA NA MKURUGENZI MTENDAJI IMF KUNDI LA KWANZA AFRIKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the IMF– for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada, mjini Marrakech, nchini Morocco, ambapo Tanzania imeeleza kuhusu kuimarika kwa uchumi wa nchi, katika Nusu ya Kwanza ya Mwaka (Januari hadi Juni, 2023), uchumi umekua kwa asilimia 5.3, ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2022.